Job 5:17-26


17 a“Heri mtu yule ambaye Mungu humrudi;
kwa hiyo usidharau adhabu yake Mwenyezi.
Mwenyezi hapa ni jina la Kiebrania Shaddai (hapa na kila mahali katika kitabu hiki cha Ayubu).

18 cKwa kuwa hutia jeraha, lakini pia huyafunga;
huumiza, lakini mikono yake pia huponya.
19 dKutoka majanga sita atakuokoa;
naam, hata katika saba hakuna dhara litakalokupata wewe.
20 eWakati wa njaa atakukomboa wewe na kifo,
naye katika vita atakukomboa na pigo la upanga.
21 fUtalindwa kutokana na kichapo cha ulimi,
wala hutakuwa na sababu ya kuogopa maangamizi yatakapokujia.
22 gUtayacheka maangamizo na njaa,
wala hutakuwa na sababu ya kuwaogopa
wanyama wakali wa mwituni.
23 hKwa kuwa utakuwa na agano na mawe ya mashamba,
nao wanyama wa mwitu watakuwa na amani nawe.
24 iUtajua ya kwamba hema lako li salama;
utahesabu mali zako wala hutakuta chochote kilichopungua.
25 jUtajua ya kuwa watoto wako watakuwa wengi,
nao wazao wako wengi kama majani ya nchi.
26 kUtaingia kaburini ukiwa na umri wa uzee mtimilifu,
kama masuke ya ngano yakusanywapo kwa wakati wake.
Copyright information for SwhNEN