‏ Job 5:19-24

19 aKutoka majanga sita atakuokoa;
naam, hata katika saba hakuna dhara litakalokupata wewe.
20 bWakati wa njaa atakukomboa wewe na kifo,
naye katika vita atakukomboa na pigo la upanga.
21 cUtalindwa kutokana na kichapo cha ulimi,
wala hutakuwa na sababu ya kuogopa maangamizi yatakapokujia.
22 dUtayacheka maangamizo na njaa,
wala hutakuwa na sababu ya kuwaogopa
wanyama wakali wa mwituni.
23 eKwa kuwa utakuwa na agano na mawe ya mashamba,
nao wanyama wa mwitu watakuwa na amani nawe.
24 fUtajua ya kwamba hema lako li salama;
utahesabu mali zako wala hutakuta chochote kilichopungua.
Copyright information for SwhNEN