Joel 1:8-13
8 aOmboleza kama bikira aliyevaa nguo ya gunia
anayehuzunika kwa ajili ya mume wa ujana wake.
9 bSadaka za nafaka na sadaka za kinywaji
zimekatiliwa mbali kutoka nyumba ya Bwana.
Makuhani wanaomboleza,
wale wanaohudumu mbele za Bwana.
10 cMashamba yameharibiwa,
ardhi imekauka;
nafaka imeharibiwa,
mvinyo mpya umekauka,
mafuta yamekoma.
11 dKateni tamaa, enyi wakulima,
lieni, enyi mlimao mizabibu;
huzunikeni kwa ajili ya ngano na shayiri,
kwa sababu mavuno ya shambani yameharibiwa.
12 eMzabibu umekauka
na mtini umenyauka;
mkomamanga, mtende na mtofaa,
miti yote shambani, imekauka.
Hakika furaha yote ya mwanadamu
imeondoka.
Wito Wa Toba
13 fVaeni nguo ya gunia, enyi makuhani, muomboleze;pigeni yowe, enyi mnaohudumu madhabahuni.
Njooni, vaeni nguo ya gunia usiku kucha,
enyi mnaohudumu mbele za Mungu wangu;
kwa kuwa sadaka za nafaka na sadaka za kinywaji
zimezuiliwa kufika katika nyumba ya Mungu wenu.
Copyright information for
SwhNEN