John 1:20-23

20 aYohana alikiri waziwazi pasipo kuficha akasema, “Mimi si Kristo.”
Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta.


21 cWakamuuliza, “Wewe ni nani basi? Je, wewe ni Eliya?”

Yeye akajibu, “Hapana, mimi siye.”

“Je, wewe ni yule Nabii?”

Akajibu, “Hapana.”

22Ndipo wakasema, “Basi tuambie wewe ni nani ili tupate jibu la kuwapelekea wale waliotutuma. Wewe wasemaje juu yako mwenyewe?”

23 dAkawajibu kwa maneno ya nabii Isaya, akisema, “Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, ‘Yanyoosheni mapito ya Bwana.’ ”

Copyright information for SwhNEN