John 12:12-16

Kuingia Kwa Yesu Yerusalemu Kwa Ushindi

(Mathayo 21:1-11; Marko 1:1-11; Luka 19:28-40)

12 aSiku iliyofuata umati mkubwa uliokuwa umekuja kwenye Sikukuu walisikia kwamba Yesu angekuja Yerusalemu. 13 bBasi wakachukua matawi ya mitende, wakatoka kwenda kumlaki, huku wakipaza sauti wakisema,

“Hosana!”
Kiebrania kusema Okoa, basi likawa neno la shangwe.


“Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Bwana!”

“Amebarikiwa Mfalme wa Israeli!”
14 dYesu akamkuta mwana-punda akampanda, kama ilivyoandikwa,

15 e“Usiogope, Ewe binti Sayuni;
tazama, Mfalme wako anakuja,
amepanda mwana-punda!”
16 fWanafunzi wake Yesu mwanzoni hawakuelewa mambo haya, lakini Yesu alipotukuzwa, ndipo walipokumbuka kuwa mambo haya yalikuwa yameandikwa kwa ajili yake na alitendewa yeye.

Copyright information for SwhNEN