John 6:66-69
66 aTangu wakati huo wafuasi wake wengi wakarejea nyuma wakaacha kumfuata.67 bHivyo Yesu akawauliza wale wanafunzi wake kumi na wawili, “Je, ninyi pia mnataka kuondoka?”
68 cSimoni Petro akamjibu, “Bwana, tuondoke twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele. 69 dTunaamini na kujua kuwa wewe ndiwe Aliye Mtakatifu wa Mungu.”
Copyright information for
SwhNEN