John 8:32-36
32 aNdipo mtaijua kweli nayo kweli itawaweka huru.”33 bWao wakamjibu, “Sisi tu wazao wa Abrahamu, nasi hatujawa watumwa wa mtu yeyote. Wawezaje kusema kwamba tutawekwa huru?”
34 cYesu akajibu, “Amin, amin nawaambia, kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi. 35 dMtumwa hakai nyumbani anakotumika siku zote, lakini mwana hukaa nyumbani daima. 36 eHivyo Mwana akiwaweka huru mtakuwa huru kweli kweli.
Copyright information for
SwhNEN