Joshua 19:40-48
Mgawo Kwa Dani
40Kura ya saba ikaangukia kabila la Dani, ukoo kwa ukoo. 41 aEneo la urithi wao lilijumuisha:Sora, Eshtaoli, Iri-Shemeshi, 42 bShaalabini, Aiyaloni, Ithla, 43 cEloni, Timna, Ekroni, 44 dElteke, Gibethoni, Baalathi, 45 eYehudi, Bene-Beraki, Gath-Rimoni, 46 fMe-Yarkoni na Rakoni, pamoja na eneo linalotazamana na Yafa.
47 g(Lakini Wadani walipata shida kulimiliki eneo lao; kwa hiyo walipanda kuishambulia Leshemu, wakaitwaa, wakawaua watu wake kwa upanga na kuukalia. Walikaa Leshemu na kuuita Dani kufuatana na jina la baba yao.)
48 hMiji hii na vijiji vyake ndio iliyokuwa urithi wa kabila la Dani, ukoo kwa ukoo.
Copyright information for
SwhNEN