Judges 20:18-28

18 aWaisraeli wakapanda Betheli na kumuuliza Mungu, “Ni nani miongoni mwetu atakayetangulia mbele yetu ili kupigana na Wabenyamini?”

Bwana akawajibu, “Yuda ndiye atakayetangulia.”

19Asubuhi yake Waisraeli wakaamka na kupiga kambi karibu na Gibea. 20Waisraeli wakatoka kupigana na Wabenyamini, nao Waisraeli wakajiweka kwenye nafasi zao katika vita dhidi yao huko Gibea. 21Wabenyamini wakatoka Gibea na kuwaua watu 22,000 wa Israeli siku ile. 22Lakini Waisraeli wakatiana moyo kila mmoja na mwenzake, nao wakajiweka kwenye nafasi zao katika vile vita mara ya pili mahali pale walipokuwa wamejiweka mara ya kwanza. 23 bWaisraeli wakapanda mbele za Bwana na kulia mbele zake mpaka jioni, nao wakamuuliza Bwana wakisema, “Je, tupande tena kupigana vita na Wabenyamini, ndugu zetu?”

Bwana akajibu, “Pandeni mkapigane nao.”

24Ndipo Waisraeli wakawakaribia Wabenyamini siku ya pili. 25Wakati huu, Wabenyamini walipotoka Gibea ili kupigana nao, wakawaua watu Waisraeli 18,000, wote wakiwa wamejifunga panga.

26 cNdipo Waisraeli, watu wote, wakapanda Betheli, huko wakakaa mbele za Bwana wakilia. Wakafunga siku ile mpaka jioni na kutoa sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya amani kwa Bwana. 27 dNao Waisraeli wakauliza kwa Bwana. (Katika siku hizo Sanduku la Agano la Mungu lilikuwa huko 28 ena Finehasi mwana wa Eleazari, mwana wa Aroni, alikuwa anahudumu mbele za hilo Sanduku.) Wakauliza, “Je, tupande kwenda vitani kupigana tena na Wabenyamini ndugu zetu, au la?”

Bwana akajibu, “Nendeni, kwa kuwa kesho nitawatia mikononi mwenu.”

Copyright information for SwhNEN