b Kum 15:21; 12:5-6, 11; Mwa 8:20; Law 6:25; 17:9; 22:19-20, 27; Ezr 8:35; Mal 1:8; Kut 12:5; Ebr 9:14; 1Pet 1:19; Hes 6:16; Isa 58:5
cKut 29:10, 15, 36; Law 4:29; 6:25; Eze 45:15; Mwa 32:20, 30; 2Nya 29:23-24; Kut 29:26; 32:30; Isa 56:7; Rum 12:1; Hes 15:25; Flp 4:18; Ebr 10:11
Leviticus 1:2-9
2 a“Sema na Waisraeli na uwaambie, ‘Yeyote miongoni mwenu aletapo sadaka ya mnyama kwa Bwana, alete mnyama kama sadaka yake kutoka kundi lake la ngʼombe au la kondoo na mbuzi.3 b“ ‘Kama sadaka hiyo ni ya kuteketezwa kutoka kwenye kundi la ngʼombe, atamtoa ngʼombe dume asiye na dosari. Ni lazima amlete kwenye ingilio la Hema la Kukutania ili aweze kukubalika kwa Bwana. 4 cAtaweka mkono wake juu ya kichwa cha sadaka ya kuteketezwa, nayo itakubaliwa kwa niaba yake ili kufanya upatanisho kwa ajili yake. 5 dAtamchinja yule fahali mchanga mbele za Bwana, kisha wana wa Aroni walio makuhani wataleta damu na kuinyunyiza pande zote za madhabahu yaliyo penye ingilio la Hema la Kukutania. 6 eAtaichuna hiyo sadaka ya kuteketezwa na kuikata vipande vipande. 7 fWana wa Aroni kuhani wataweka moto juu ya madhabahu na kupanga kuni juu ya huo moto. 8 gKisha wana wa Aroni walio makuhani watapanga vile vipande vya nyama, pamoja na kichwa na mafuta ya huyo mnyama juu ya zile kuni zinazowaka juu ya madhabahu. 9 hAtaziosha sehemu za ndani na miguu yake kwa maji, naye kuhani atavichoma vyote juu ya madhabahu. Hii ni sadaka ya kuteketezwa, sadaka iliyotolewa kwa moto, yenye harufu nzuri ya kumpendeza Bwana.
Copyright information for
SwhNEN