bKum 11:14; 28:12; Za 65:9; 67:6; 68:9; 104:13; 147:8; Yer 5:24; Hos 6:3; Yoe 2:23; Zek 10:1; Ay 5:10; 14:9; Kut 23:24; Law 25:19
d Za 3:5; 4:8; 29:11; 37:11; 85:8; 147:14; Isa 17:2; 26:3; 54:13; 60:18; Hag 2:9; Mit 3:24; Ay 11:18-19; Yer 30:10; Mik 4:4; Sef 3:13; Mwa 37:20
Leviticus 26:3-13
3 a“ ‘Ikiwa mtafuata amri zangu na kuwa waangalifu kutii maagizo yangu, 4 bnitawanyeshea mvua katika majira yake, nayo ardhi itatoa mazao yake, na miti ya mashambani itazaa matunda yake. 5 cKupura nafaka kwenu kutaendelea mpaka wakati wa kuvuna zabibu. Pia kuvuna zabibu kutaendelea mpaka wakati wa kupanda mbegu, nanyi mtakula na kushiba, na mtaishi salama katika nchi yenu.6 d“ ‘Nitawapa amani katika nchi, mpate kulala pasipo kutiwa hofu na yeyote. Nitawaondoa wanyama wakali watoke kwenye nchi, nao upanga hautapita katika nchi yenu. 7 eMtawafukuza adui zenu, nanyi mtawaua kwa upanga mbele yenu. 8 fWatu wenu watano watafukuza adui mia, watu wenu mia watafukuza adui elfu kumi, nao adui zenu wataanguka kwa upanga mbele yenu.
9 g“ ‘Nitawaangalia kwa upendeleo na kuwafanya mzae na kuzidisha idadi yenu, nami nitalishika Agano langu na ninyi. 10 hWakati wa kuvuna mtakuwa bado mnakula mavuno ya mwaka uliopita, na itawalazimu kuyaondoa ghalani ili mpate nafasi ya mavuno mapya. 11 iNitafanya makao yangu miongoni mwenu, nami sitawachukia. 12 jNitatembea katikati yenu niwe Mungu wenu, nanyi mtakuwa watu wangu. 13 kMimi ndimi Bwana Mungu wenu, niliyewatoa katika nchi ya Misri ili msiendelee kuwa watumwa wa Wamisri, nikavunja kongwa lenu, na kuwawezesha kutembea mkiwa mmeinua vichwa vyenu juu.
Copyright information for
SwhNEN