Luke 18:31-33

Yesu Atabiri Kifo Chake Mara Ya Tatu

(Mathayo 20:17-19; Marko 10:32-34)

31 aYesu akawachukua wale wanafunzi wake kumi na wawili kando na kuwaambia, “Tunapanda kwenda Yerusalemu, na kila kitu kilichoandikwa na manabii kumhusu Mwana wa Adamu kitatimizwa. 32 bKwa kuwa atatiwa mikononi mwa watu wasiomjua Mungu, nao watamdhihaki, watamtukana na kumtemea mate, watampiga mijeledi na kumuua. 33 cNaye siku ya tatu atafufuka.”

Copyright information for SwhNEN