Luke 20:41-44
Kristo Ni Mwana Wa Nani?
(Mathayo 22:41-46; Marko 12:35-37)
41 a bKisha Yesu akawaambia, “Imekuwaje basi wao husema Kristo ▼▼Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta.
ni Mwana wa Daudi? 42 dDaudi mwenyewe anasema katika Kitabu cha Zaburi:“ ‘Bwana alimwambia Bwana wangu:
“Keti mkono wangu wa kuume,
43 e hadi nitakapowaweka adui zako
chini ya miguu yako.” ’
44 Ikiwa Daudi anamwita yeye ‘Bwana,’ basi atakuwaje mwanawe?”
Copyright information for
SwhNEN