Luke 21:1-4
Sadaka Ya Mjane
(Marko 12:41-44)
1 aYesu alipoinua macho yake, aliwaona matajiri wakiweka sadaka zao kwenye sanduku la hazina ya Hekalu. 2Akamwona pia mjane mmoja maskini akiweka humo sarafu mbili ndogo za shaba. 3 bYesu akasema, “Amin, nawaambia, huyu mjane maskini ameweka humo zaidi ya watu wengine wote. 4 cHawa watu wengine wote wametoa sadaka kutokana na wingi wa mali zao. Lakini huyu mjane ametoa kutokana na umaskini wake vyote alivyokuwa navyo, hata kile alichohitaji ili kuishi.”
Copyright information for
SwhNEN