Luke 22:66-71
Yesu Apelekwa Mbele Ya Baraza
(Mathayo 26:59-66; Marko 14:55-64; Yohana 18:28-38)
66 aKulipopambazuka, baraza la wazee wa watu, ▼▼Baraza la wazee hapa ina maana ya Sanhedrin ambalo lilikuwa ndilo Baraza la juu kabisa la utawala wa Kiyahudi, lililoundwa na wazee 70 pamoja na kuhani mkuu.
yaani viongozi wa makuhani na walimu wa sheria, wakakutana pamoja, naye Yesu akaletwa mbele yao. 67 cWakamwambia, “Kama wewe ndiye Kristo, ▼▼Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta.
tuambie.”Yesu akawajibu, “Hata nikiwaambia hamtaamini. 68 eNami nikiwauliza swali, hamtanijibu. 69 fLakini kuanzia sasa, Mwana wa Adamu ataketi mkono wa kuume wa Mungu Mwenye Nguvu.”
70 gWote wakauliza, “Wewe basi ndiwe Mwana wa Mungu?”
Yeye akawajibu, “Ninyi mwasema kwamba mimi ndiye.”
71 hKisha wakasema, “Tuna haja gani tena ya ushahidi zaidi? Tumesikia wenyewe kutoka kinywani mwake.”
Copyright information for
SwhNEN