Luke 23:1-5
Yesu Apelekwa Kwa Pilato
(Mathayo 27:1-14; Marko 15:1-5; Yohana 18:28-38)
1 aKisha umati wote wa watu ukainuka na kumpeleka Yesu kwa Pilato. 2 bNao wakaanza kumshtaki wakisema: “Tumemwona huyu mtu akipotosha taifa letu, akiwazuia watu wasilipe kodi kwa Kaisari na kujiita kuwa yeye ni Kristo, ▼▼Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta.
mfalme.” 3 dBasi Pilato akamuuliza Yesu, “Wewe ndiye mfalme wa Wayahudi?”
Yesu akajibu, “Wewe wasema.”
4 ePilato akawaambia viongozi wa makuhani na watu wote waliokuwepo, “Sioni sababu ya kutosha kumshtaki mtu huyu!”
5 fLakini wao wakakazana kusema, “Anawachochea watu kwa mafundisho yake katika Uyahudi yote, tangu Galilaya alikoanzia, hadi sehemu hii!”
Copyright information for
SwhNEN