Luke 24:34-43
34 awakisema, “Ni kweli! Bwana amefufuka, naye amemtokea Simoni.” 35 bKisha wale wanafunzi wawili wakaeleza yaliyotukia njiani na jinsi walivyomtambua Yesu alipoumega mkate.Yesu Awatokea Wanafunzi Wake
(Mathayo 28:16-20; Marko 16:14-18; Yohana 20:19-23; Matendo 1:6-8)
36 cWalipokuwa bado wanazungumza hayo, Yesu mwenyewe akasimama katikati yao, akasema, “Amani iwe nanyi!”37 dWakashtuka na kuogopa wakidhani kwamba wameona mzuka. 38Lakini Yesu akawauliza, “Kwa nini mnaogopa? Kwa nini mna shaka mioyoni mwenu? 39 eTazameni mikono yangu na miguu yangu, mwone kuwa ni mimi hasa. Niguseni mwone; kwa maana mzuka hauna nyama na mifupa, kama mnionavyo kuwa navyo.”
40Aliposema haya, akawaonyesha mikono na miguu yake. 41 fWakashindwa kuamini kwa ajili ya furaha na mshangao waliokuwa nao. Akawauliza, “Mna chakula chochote hapa?”
42Wakampa kipande cha samaki aliyeokwa, 43 gnaye akakichukua na kukila mbele yao.
Copyright information for
SwhNEN