Luke 9:18-21

Petro Amkiri Yesu Kuwa Ndiye Kristo

(Mathayo 16:13-19; Marko 8:27-29)

18 aWakati mmoja, Yesu alipokuwa akiomba faraghani, nao wanafunzi wake wakiwa pamoja naye, akawauliza, “Watu husema mimi ni nani?”

19 bWakamjibu, “Baadhi husema wewe ni Yohana Mbatizaji, wengine husema ni Eliya, na bado wengine husema kwamba ni mmoja wa manabii wa kale amefufuka kutoka kwa wafu.”

20 cKisha akawauliza, “Je, ninyi mnasema mimi ni nani?”

Petro akajibu, “Wewe ndiwe Kristo
Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta.
wa Mungu.”

21 eYesu akawakataza wasimwambie mtu yeyote jambo hilo.
Copyright information for SwhNEN