Mark 1:1-8

Mahubiri Ya Yohana Mbatizaji

(Mathayo 3:1-12; Luka 3:1-8; Yohana 1:19-28)

1 aMwanzo wa Injili ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu.

2 bKama ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya:

“Tazama, nitamtuma mjumbe wangu mbele yako,
atakayetengeneza njia mbele yako”:
3 c“sauti ya mtu aliaye nyikani.
‘Itengenezeni njia ya Bwana,
yanyoosheni mapito yake.’ ”
4 dYohana alikuja, akibatiza huko nyikani, akihubiri ubatizo wa toba kwa ajili ya msamaha wa dhambi. 5 eWatu kutoka Uyahudi wote na sehemu zote za Yerusalemu walikuwa wakimwendea. Nao wakaziungama dhambi zao, akawabatiza katika Mto Yordani. 6 fYohana alivaa mavazi yaliyotengenezwa kwa singa za ngamia na mkanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwitu. 7 gNaye alihubiri akisema, “Baada yangu atakuja yeye aliye na uwezo kuniliko mimi, ambaye sistahili hata kuinama na kulegeza kamba za viatu vyake. 8 hMimi nawabatiza kwa maji, lakini yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu.”

Copyright information for SwhNEN