‏ Mark 13:24-31

Kuja Kwa Mwana Wa Adamu

(Mathayo 24:29-31; Luka 21:25-28)

24 a “Lakini katika siku hizo, baada ya hiyo dhiki,

“ ‘jua litatiwa giza
nao mwezi hautatoa nuru yake;
25 b nazo nyota zitaanguka kutoka angani,
na nguvu za anga zitatikisika.’
26 c “Ndipo watu wote watakapomwona Mwana wa Adamu akija mawinguni kwa nguvu nyingi na utukufu. 27 dNaye atawatuma malaika wake wawakusanye wateule wake kutoka pande zote nne za dunia, kutoka miisho ya dunia hadi miisho ya mbingu.

Somo Kuhusu Mtini

(Mathayo 24:32-35; Luka 21:29-33)

28 e “Basi jifunzeni somo hili kutokana na mtini: Matawi yake yanapoanza kuchipua na kutoa majani, mnatambua kwamba wakati wa kiangazi umekaribia. 29Vivyo hivyo, myaonapo mambo haya yakitukia, mnatambua kwamba wakati u karibu, hata malangoni. 30 fAmin, nawaambia, kizazi hiki hakitapita hadi mambo haya yote yawe yametimia. 31 gMbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.

Copyright information for SwhNEN