Mark 6:1-6
Nabii Hana Heshima Kwao
(Mathayo 13:53-58; Luka 4:16-30)
1 aYesu akaondoka huko na kwenda mji wa kwao, akiwa amefuatana na wanafunzi wake. 2 bIlipofika siku ya Sabato, akaanza kufundisha katika sinagogi, na wengi waliomsikia wakashangaa.Nao wakauliza, “Mtu huyu ameyapata wapi mambo haya yote? Tazama ni hekima ya namna gani hii aliyopewa? Tazama matendo ya miujiza ayafanyayo kwa mikono yake! 3 cHuyu si yule seremala, mwana wa Maria? Na ndugu zake si Yakobo, Yose, ▼
▼Yosefu kwa Kiyunani ni Joses.
Yuda na Simoni? Dada zake wote si tuko nao hapa kwetu?” Nao wakachukizwa sana kwa ajili yake, wakakataa kumwamini. 4 eYesu akawaambia, “Nabii hakosi heshima isipokuwa katika mji wake mwenyewe, na miongoni mwa jamaa na ndugu zake, na nyumbani kwake.” 5 fHakufanya miujiza yoyote huko isipokuwa kuweka mikono yake juu ya wagonjwa wachache na kuwaponya. 6 gNaye akashangazwa sana kwa jinsi wasivyokuwa na imani.
Yesu Awatuma Wale Kumi Na Wawili
(Mathayo 10:5-15; Luka 9:1-6)
Kisha Yesu akawa anakwenda kutoka kijiji kimoja hadi kingine akifundisha.
Copyright information for
SwhNEN