Mark 6:7-13
7 aAkawaita wale kumi na wawili, akawatuma wawili wawili, na kuwapa mamlaka kutoa pepo wachafu.8Akawaagiza akisema, “Msichukue chochote kwa ajili ya safari isipokuwa fimbo tu. Msichukue mkate, wala mkoba, wala fedha kwenye mikanda yenu. 9 bVaeni viatu, lakini msivae nguo ya ziada.” 10 cAkawaambia, “Mkiingia kwenye nyumba yoyote, kaeni humo hadi mtakapoondoka katika mji huo. 11 dKama mahali popote hawatawakaribisha wala kuwasikiliza, mtakapoondoka huko, kungʼuteni mavumbi kutoka kwenye miguu yenu ili kuwa ushuhuda dhidi yao.”
12 eKwa hiyo wakatoka na kuhubiri kwamba inawapasa watu kutubu na kuacha dhambi. 13 fWakatoa pepo wachafu wengi, wakawapaka wagonjwa wengi mafuta na kuwaponya.
Copyright information for
SwhNEN