Mark 9:38-40
Yeyote Asiye Kinyume Nasi Yuko Upande Wetu
(Luka 9:49-50)
38 aYohana akamwambia, “Mwalimu, tumemwona mtu akitoa pepo wachafu kwa jina lako, nasi tukamkataza, kwa sababu yeye si mmoja wetu.”39 bYesu akasema, “Msimkataze, kwa kuwa hakuna yeyote atendaye miujiza kwa Jina langu ambaye baada ya kitambo kidogo aweza kunena lolote baya dhidi yangu. 40 cKwa maana yeyote asiye kinyume chetu, yuko upande wetu.
Copyright information for
SwhNEN