Matthew 13:53-58
Yesu Akataliwa Nazareti
(Marko 6:1-6; Luka 4:16-30)
53 aYesu alipomaliza kutoa mifano hii, akaondoka. 54 bAlipofika mji wa kwao, akawafundisha watu katika sinagogi lao. Nao wakastaajabu, wakauliza, “Mtu huyu amepata wapi hekima hii na uwezo huu wa kufanya miujiza?” 55 c“Huyu si yule mwana wa seremala? Mama yake si yeye aitwaye Maria, nao ndugu zake si Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? 56 dNao dada zake wote, hawako hapa pamoja nasi? Mtu huyu amepata wapi basi mambo haya yote?” 57 eWakachukizwa naye.Lakini Yesu akawaambia, “Nabii hakosi heshima, isipokuwa katika nchi yake na nyumbani kwake.”
58 fNaye hakufanya miujiza mingi huko kwa sababu ya kutokuamini kwao.
Copyright information for
SwhNEN