Matthew 14:13-21
Yesu Alisha Wanaume 5,000
(Marko 6:30-44; Luka 9:10-17; Yohana 6:1-14)
13 aYesu aliposikia yaliyokuwa yametukia, aliondoka kwa chombo akaenda mahali pasipo na watu ili awe peke yake. Lakini watu walipopata habari, wakamfuata kwa miguu kupitia nchi kavu kutoka miji. 14 bYesu alipofika kando ya bahari, aliona makutano makubwa ya watu, akawahurumia na akawaponya wagonjwa wao.15 cIlipofika jioni, wanafunzi wake walienda kwake, wakamwambia, “Mahali hapa ni nyikani, na muda sasa umekwisha. Waage makutano ili waende zao vijijini wakajinunulie chakula.”
16Yesu akawaambia, “Hakuna sababu ya wao kuondoka. Ninyi wapeni chakula.”
17 dWakamjibu, “Tuna mikate mitano na samaki wawili tu.”
18Akawaambia, “Nileteeni hivyo vitu hapa.” 19 eYesu akaagiza makutano wakae chini kwenye nyasi. Akaichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili, akainua macho yake akatazama mbinguni, akavibariki na kuimega ile mikate. Kisha akawapa wanafunzi, nao wanafunzi wakawagawia makutano. 20 fWote wakala, wakashiba. Nao wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia, wakajaza vikapu kumi na viwili. 21Idadi ya watu waliokula walikuwa wanaume wapatao 5,000, bila kuhesabu wanawake na watoto.
Copyright information for
SwhNEN