Matthew 21:1-9
Yesu Anaingia Yerusalemu Kwa Shangwe
(Marko 11:1-11; Luka 19:28-40; Yohana 12:12-19)
1 aWalipokaribia Yerusalemu, wakafika Bethfage katika Mlima wa Mizeituni. Ndipo Yesu akawatuma wanafunzi wake wawili, 2akawaambia, “Nendeni katika kijiji kilichoko mbele yenu, nanyi mtamkuta punda amefungwa hapo, na mwana-punda pamoja naye. Wafungueni na mniletee. 3 bKama mtu yeyote akiwasemesha lolote, mwambieni kwamba Bwana ana haja nao, naye atawaruhusu mwalete mara.”4 cHaya yalitukia ili litimie lile lililonenwa na nabii, akisema:
5 d“Mwambieni Binti Sayuni,
‘Tazama, mfalme wako anakuja kwako,
ni mnyenyekevu, naye amepanda punda,
juu ya mwana-punda, mtoto wa punda.’ ”
6 eWale wanafunzi wakaenda, wakafanya kama Yesu alivyokuwa amewaagiza. 7 fWakamleta yule punda na mwana-punda, nao wakatandika mavazi yao juu ya hao punda, naye Yesu akaketi juu yake. 8 gUmati mkubwa wa watu ukatandaza mavazi yao barabarani, na wengine wakakata matawi kutoka kwenye miti, wakayatandaza barabarani. 9 hUle umati wa watu uliomtangulia na ule uliomfuata ukapiga kelele ukisema,
“Hosana, ▼
▼Kiebrania kusema Okoa, basi likawa neno la shangwe.
Mwana wa Daudi!”“Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Bwana!”
“Hosana juu mbinguni!”
Copyright information for
SwhNEN