Matthew 24:42-46
42 a “Basi kesheni, kwa sababu hamjui ni siku gani atakapokuja Bwana wenu. 43 bLakini fahamuni jambo hili: Kama mwenye nyumba angejua ni wakati gani wa usiku ambao mwizi atakuja, angekesha na hangekubali nyumba yake kuvunjwa. 44 cKwa hiyo ninyi pia hamna budi kuwa tayari, kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja saa msiyotazamia.Mfano Wa Mtumishi Mwaminifu
(Luka 12:41-48)
45 d “Ni nani basi aliye mtumishi mwaminifu na mwenye busara, ambaye bwana wake amemweka kusimamia watumishi wengine katika nyumba yake, ili awape chakula chao kwa wakati unaofaa? 46 eHeri mtumishi yule ambaye bwana wake atakaporudi atamkuta akifanya hivyo.
Copyright information for
SwhNEN