Matthew 26:1-5
Shauri Baya La Kumuua Yesu
(Marko 14:1-2; Luka 22:1-2; Yohana 11:45-53)
1 aYesu alipomaliza kusema hayo yote, akawaambia wanafunzi wake, 2 b“Kama mnavyojua, baada ya siku mbili itakuwa Pasaka, naye Mwana wa Adamu atasalitiwa ili asulubiwe.”3 cBasi viongozi wa makuhani na wazee wa watu wakakusanyika katika jumba la utawala la kuhani mkuu, jina lake Kayafa. 4 dWakafanya shauri ili kumkamata Yesu kwa siri na kumuua. 5 eLakini wakasema, “Isiwe wakati wa Sikukuu, kusitokee ghasia miongoni mwa watu.”
Copyright information for
SwhNEN