Matthew 26:59-61
59 aViongozi wa makuhani na Baraza la Wayahudi lote wakatafuta ushahidi wa uongo dhidi ya Yesu ili wapate kumuua. 60 bLakini hawakupata jambo lolote, ingawa mashahidi wengi wa uongo walijitokeza.Hatimaye wakajitokeza mashahidi wawili wa uongo 61 cna kusema, “Huyu mtu alisema, ‘Ninaweza kulivunja Hekalu la Mungu na kulijenga tena kwa siku tatu.’ ”
Copyright information for
SwhNEN