Matthew 27:11-14
Yesu Mbele Ya Pilato
(Marko 15:2-15; Luka 23:3-25; Yohana 18:33–19:16)
11 aWakati huo Yesu akiwa amesimama mbele ya mtawala, mtawala akamuuliza, “Wewe ndiye mfalme wa Wayahudi?”Yesu akasema, “Wewe wasema hivyo.”
12 bLakini viongozi wa makuhani na wazee walipomshtaki, hakujibu neno. 13 cNdipo Pilato akamuuliza, “Je, husikii ni mambo mangapi wanayokushtaki nayo?” 14 dLakini Yesu hakumjibu hata kwa shtaka moja, kiasi kwamba mtawala alishangaa sana.
Copyright information for
SwhNEN