Matthew 7:16-20
16 aMtawatambua kwa matunda yao. Je, watu huchuma zabibu kwenye miiba, au tini kwenye michongoma? 17 bVivyo hivyo, mti mwema huzaa matunda mazuri, na mti mbaya huzaa matunda mabaya. 18 cMti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mbaya hauwezi kuzaa matunda mazuri. 19 dKila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni. 20Hivyo, mtawatambua kwa matunda yao.
Copyright information for
SwhNEN