Matthew 8:14-17
Yesu Aponya Wengi
(Marko 1:29-34; Luka 4:38-41)
14 aYesu alipoingia nyumbani kwa Petro, alimkuta mama mkwe wa Petro amelala kitandani, akiwa ana homa. 15 bAkamgusa mkono wake na homa ikamwacha, naye akainuka na kuanza kumhudumia.16 cJioni ile, wakamletea watu wengi waliopagawa na pepo wachafu, naye akawatoa wale pepo wachafu kwa neno lake, na kuwaponya wagonjwa wote. 17 dHaya yalifanyika ili litimie lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Isaya kwamba:
“Mwenyewe alitwaa udhaifu wetu
na alichukua magonjwa yetu.”
Copyright information for
SwhNEN