Matthew 8:23-27
Yesu Atuliza Dhoruba
(Marko 4:35-41; Luka 8:22-25)
23 aNaye alipoingia kwenye mashua, wanafunzi wake wakamfuata. 24 bGhafula, kukainuka dhoruba kali baharini hata mashua ikaanza kufunikwa na mawimbi, lakini Yesu alikuwa amelala usingizi. 25Wanafunzi wake wakamwendea na kumwamsha, wakisema, “Bwana, tuokoe! Tunazama!”26 cNaye Yesu akawaambia, “Kwa nini mnaogopa, enyi wa imani haba?” Kisha akaamka na kukemea dhoruba na mawimbi, nako kukawa shwari kabisa.
27Wale watu wakashangaa, wakisema, “Ni mtu wa namna gani huyu? Hata upepo na mawimbi vinamtii!”
Copyright information for
SwhNEN