Nehemiah 11:15-19

15Kutoka Walawi:

Shemaya mwana wa Hashubu, mwana wa Azrikamu, mwana wa Hashabia, mwana wa Buni;
16 aShabethai na Yozabadi, viongozi wawili wa Walawi, ambao walisimamia kazi za nje za nyumba ya Mungu; 17 bMatania mwana wa Mika, mwana wa Zabdi, mwana wa Asafu, kiongozi aliyeongoza kutoa shukrani na maombi; Bakbukia aliyekuwa msaidizi wake kati ya wenzake; na Abda mwana wa Shamua, mwana wa Galali, mwana wa Yeduthuni. 18 cJumla ya Walawi waliokaa katika mji mtakatifu walikuwa watu 284.

19 dMabawabu:

Akubu, Talmoni na wenzao, waliolinda malango: watu 172.

Copyright information for SwhNEN