Numbers 15:1-7
Sadaka Za Nyongeza
1 Bwana akamwambia Mose, 2 a“Sema na Waisraeli uwaambie: ‘Baada ya ninyi kuingia katika nchi ninayowapa kama nyumbani, 3 bnanyi mkitoa sadaka za kuteketezwa kwa moto, kutoka makundi ya ngʼombe au kondoo, kama harufu nzuri inayompendeza Bwana, ikiwa ni sadaka za kuteketezwa au dhabihu, kwa ajili ya nadhiri maalum ama sadaka ya hiari au sadaka ya sikukuu zenu, 4 cndipo yeye aletaye sadaka yake ataiweka mbele za Bwana sadaka ya nafaka, sehemu ya kumi ya efa ▼▼Sehemu ya kumi ya efa ni sawa na kilo moja.
ya unga laini uliochanganywa na robo ya hini ▼▼Robo ya hini ni sawa na lita moja.
ya mafuta. 5 fPamoja na kila mwana-kondoo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa au dhabihu, andaa robo ya hini ya divai kwa sadaka ya kinywaji. 6 g“ ‘Pamoja na kondoo dume andaa sadaka ya nafaka ya sehemu mbili za kumi za efa ▼
▼Sehemu mbili za kumi za efa ni sawa na kilo 2.
za unga laini uliochanganywa na theluthi moja ▼▼Theluthi moja ya hini ni sawa na lita moja na nusu.
ya hini ya mafuta, 7 jna theluthi moja ya hini ya divai kama sadaka ya kinywaji. Vitoe kama harufu nzuri inayompendeza Bwana.
Copyright information for
SwhNEN