Numbers 4:35-40
35Wanaume wote kuanzia umri wa miaka thelathini hadi hamsini ambao walikuja kutumika katika Hema la Kukutania, 36waliohesabiwa kwa koo zao, walikuwa 2,750. 37 aHii ilikuwa ndiyo jumla ya wote wale wa koo za Wakohathi ambao walitumika katika Hema la Kukutania. Mose na Aroni waliwahesabu kufuatana na amri ya Bwana kupitia kwa Mose.38 bWagershoni walihesabiwa kwa koo zao na jamaa zao. 39Watu wote kuanzia umri wa miaka thelathini hadi hamsini ambao walikuja kutumika katika Hema la Kukutania, 40waliohesabiwa kwa koo zao na jamaa zao, walikuwa 2,630.
Copyright information for
SwhNEN