Numbers 9:2-5
2 a“Waamuru Waisraeli waadhimishe Pasaka katika wakati ulioamriwa. 3 bAdhimisheni wakati ulioamriwa, yaani wakati wa kuzama jua siku ya kumi na nne ya mwezi huu, kufuatana na desturi zake zote na masharti yake.”4 cHivyo Mose akawaambia Waisraeli waiadhimishe Pasaka, 5 dnao wakafanya hivyo kwenye Jangwa la Sinai wakati wa kuzama jua siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza. Waisraeli wakafanya kila kitu kama vile Bwana alivyomwamuru Mose.
Copyright information for
SwhNEN