Proverbs 18:20-24


20 aTumbo la mtu litajaa kutokana na tunda la kinywa chake,
atashibishwa mavuno yanayotokana na midomo yake.

21 bMauti na uzima viko katika uwezo wa ulimi,
nao waupendao watakula matunda yake.

22 cApataye mke apata kitu chema
naye ajipatia kibali kwa Bwana.

23 dMtu maskini huomba kuhurumiwa
bali tajiri hujibu kwa ukali.

24 eMtu mwenye marafiki wengi wanaweza kumharibu,
bali yuko rafiki aambatanaye na mtu kwa karibu kuliko ndugu.
Copyright information for SwhNEN