Proverbs 23:29-35


29 aNi nani mwenye ole?
Ni nani mwenye huzuni?
Ni nani mwenye ugomvi?
Ni nani mwenye malalamiko?
Ni nani aliye na majeraha yasiyo na sababu?
Ni nani mwenye macho mekundu?
30 bNi hao wakaao sana kwenye mvinyo,
hao waendao kuonja mabakuli ya mvinyo uliochanganywa.
31Usiukodolee macho mvinyo wakati ukiwa mwekundu,
wakati unapometameta kwenye bilauri,
wakati ushukapo taratibu!
32Mwishowe huuma kama nyoka
na kutia sumu yake kama nyoka mwenye sumu.
33Macho yako yataona mambo mageni
na moyo wako kuwazia mambo yaliyopotoka.
34Utakuwa kama alalaye katikati ya bahari,
alalaye juu ya kamba ya merikebu.
35 cUtasema, “Wamenipiga lakini sikuumia!
Wamenichapa, lakini sisikii!
Nitaamka lini
ili nikanywe tena?”
Copyright information for SwhNEN