Proverbs 26:13-16


13 aMvivu husema, “Yuko simba barabarani,
simba mkali anazunguka mitaa!”

14 bKama vile mlango ugeukavyo kwenye bawaba zake,
ndivyo mvivu ajigeuzavyo kitandani mwake.

15 cMtu mvivu hutumbukiza mkono wake kwenye sahani,
naye huchoka kuupeleka kwenye kinywa chake.

16Mtu mvivu ni mwenye hekima machoni pake mwenyewe,
kuliko watu saba wawezao kujibu kwa busara.
Copyright information for SwhNEN