Proverbs 27:23-27


23 aHakikisha kuwa unajua hali ya makundi yako
ya kondoo na mbuzi,
angalia kwa bidii ngʼombe zako.
24 bKwa kuwa utajiri haudumu milele,
nayo taji haidumu vizazi vyote.
25 cWakati majani makavu yameondolewa
na mapya yamechipua,
nayo majani toka milimani yamekusanywa,
26wana-kondoo watakupatia mavazi
na mbuzi thamani ya shamba.
27Utakuwa na maziwa mengi ya mbuzi
kukulisha wewe na jamaa yako,
na kuwalisha watumishi wako wa kike.
Copyright information for SwhNEN