Proverbs 3:21-26


21 aMwanangu, hifadhi maamuzi mema na busara,
usiache vitoke machoni pako;
22 bndipo vitakapokuwa uzima nafsini mwako
na pambo la neema shingoni mwako.
23Kisha utaenda katika njia yako salama,
wala mguu wako hautajikwaa;
24 culalapo, hautaogopa;
ulalapo usingizi wako utakuwa mtamu.

25 dUsiogope maafa ya ghafula
au maangamizi yanayowapata waovu,
26 ekwa kuwa Bwana atakuwa tumaini lako
na kuepusha mguu wako kunaswa katika mtego.
Copyright information for SwhNEN