Proverbs 30:7-9


7“Ninakuomba vitu viwili, Ee Bwana;
usininyime kabla sijafa:
8 aUutenge mbali nami udanganyifu na uongo;
usinipe umaskini wala utajiri,
bali unipe chakula cha kunitosha kila siku.
9 bNisije nikawa na vingi vya kuzidi nikakukana
na kusema, ‘Bwana ni nani?’
Au nisije nikawa maskini nikaiba,
nami nikaliaibisha jina la Mungu wangu.
Copyright information for SwhNEN