Proverbs 31:4-7


4 a“Ee Lemueli, haifai wafalme,
haifai wafalme kunywa mvinyo,
haifai watawala kutamani sana kileo,
5 bwasije wakanywa na kusahau vile sheria inavyoamuru
na kuwanyima haki zao wote walioonewa.
6 cWape kileo wale wanaoangamia,
mvinyo wale walio na uchungu,
7 dWanywe na kusahau umaskini wao
na wasikumbuke taabu yao tena.
Copyright information for SwhNEN