Proverbs 6:20-29
Onyo Dhidi Ya Uasherati
20 aMwanangu, zishike amri za baba yako,wala usiyaache mafundisho ya mama yako.
21 bYafunge katika moyo wako daima,
yakaze kuizunguka shingo yako.
22 cWakati utembeapo, yatakuongoza;
wakati ulalapo, yatakulinda;
wakati uamkapo, yatazungumza nawe.
23 dKwa maana amri hizi ni taa,
mafundisho haya ni mwanga
na maonyo ya maadili ni njia ya uzima,
24 eyakikulinda na mwanamke aliyepotoka,
kutokana na maneno laini ya mwanamke aliyepotoka.
25 fMoyo wako usitamani uzuri wake
wala macho yake yasikuteke,
26 gkwa maana kahaba atakufanya uwe maskini,
hata ukose kipande cha mkate,
naye mwanamke mzinzi huwinda maisha yako hasa.
27Je, mtu aweza kuchotea moto kwenye paja lake
bila nguo zake kuungua?
28Je, mtu aweza kutembea juu ya makaa ya moto yanayowaka
bila miguu yake kuungua?
29 hNdivyo alivyo mtu alalaye na mke wa mwanaume mwingine;
hakuna yeyote amgusaye huyo mwanamke ambaye hataadhibiwa.
Copyright information for
SwhNEN