Proverbs 8

Wito Wa Hekima

1 aJe, hekima haitani?
Je, ufahamu hapazi sauti?
2Juu ya miinuko karibu na njia,
penye njia panda, ndipo asimamapo;
3 bkando ya malango yaelekeayo mjini,
kwenye maingilio, hulia kwa sauti kubwa, akisema:
4 c“Ni ninyi wanaume, ninaowaita;
ninapaza sauti yangu kwa wanadamu wote.
5 dNinyi ambao ni wajinga, pateni akili;
ninyi mlio wapumbavu, pateni ufahamu.
6 eSikilizeni, kwa maana nina mambo muhimu ya kusema;
ninafungua midomo yangu kusema lililo sawa.
7 fKinywa changu husema lililo kweli,
kwa maana midomo yangu huchukia uovu.
8Maneno yote ya kinywa changu ni haki;
hakuna mojawapo lililopotoka wala ukaidi.
9Kwa wenye kupambanua yote ni sahihi;
hayana kasoro kwa wale wenye maarifa.
10 gChagua mafundisho yangu badala ya fedha,
maarifa badala ya dhahabu safi,
11 hkwa maana hekima ina thamani kuliko marijani
na hakuna chochote unachohitaji kinacholingana naye.

12 i“Mimi hekima, nakaa pamoja na busara;
ninamiliki maarifa na busara.
13 jKumcha Bwana ni kuchukia uovu;
ninachukia kiburi na majivuno,
tabia mbaya na mazungumzo potovu.
14 kUshauri na hukumu sahihi ni vyangu;
nina ufahamu na nina nguvu.
15 lKwa msaada wangu wafalme hutawala
na watawala hutunga sheria zilizo za haki,
16 mkwa msaada wangu wakuu hutawala,
na wenye vyeo wote watawalao dunia.
17 nNawapenda wale wanipendao,
na wale wanitafutao kwa bidii wataniona.
18 oUtajiri na heshima viko kwangu,
utajiri udumuo na mafanikio.
19 pTunda langu ni bora kuliko dhahabu safi;
kile nitoacho hupita fedha iliyo bora.
20Natembea katika njia ya unyofu
katika mapito ya haki,
21 qnawapa utajiri wale wanipendao
na kuzijaza hazina zao.

22 rBwana aliniumba mwanzoni mwa kazi yake,
kabla ya matendo yake ya zamani;
23 sniliteuliwa tangu milele,
tangu mwanzoni, kabla ya dunia kuumbwa.
24 tWakati hazijakuwepo bahari, nilikwishazaliwa,
wakati hazijakuwepo chemchemi zilizojaa maji;
25 ukabla milima haijawekwa mahali pake,
kabla vilima havijakuwepo, nilikwishazaliwa,
26 vkabla hajaumba dunia wala mashamba yake
au vumbi lolote la dunia.
27 wNilikuwepo alipoziweka mbingu mahali pake,
wakati alichora mstari wa upeo wa macho
juu ya uso wa kilindi,
28 xwakati aliweka mawingu juu
na kuziweka imara chemchemi za bahari,
29 ywakati aliiwekea bahari mpaka wake
ili maji yasivunje agizo lake,
na wakati aliweka misingi ya dunia.
30Wakati huo nilikuwa fundi stadi kando yake.
Nilijazwa na furaha siku baada ya siku,
nikifurahi daima mbele zake,
31 znikifurahi katika dunia yake yote
nami nikiwafurahia wanadamu.

32 aa“Basi sasa wanangu, nisikilizeni;
heri wale wanaozishika njia zangu.
33Sikilizeni mafundisho yangu mwe na hekima;
msiyapuuze.
34 abHeri mtu yule anisikilizaye mimi,
akisubiri siku zote malangoni mwangu,
akingoja kwenye vizingiti vya mlango wangu.
35 acKwa maana yeyote anipataye mimi amepata uzima
na kujipatia kibali kutoka kwa Bwana.
36 adLakini yeyote ashindwaye kunipata
hujiumiza mwenyewe;
na wote wanichukiao mimi hupenda mauti.”
Copyright information for SwhNEN