Psalms 101

Ahadi Ya Kuishi Kwa Uadilifu Na Kwa Haki

Zaburi ya Daudi.

1 aNitaimba juu ya upendo wako na haki yako;
kwako wewe, Ee Bwana, nitaimba sifa.
2 bNitazingatia kuishi maisha yasiyo na lawama:
utakuja kwangu lini?

Nitatembea nyumbani mwangu
kwa moyo usio na lawama.
3 cSitaweka mbele ya macho yangu
kitu kiovu.

Ninayachukia matendo ya watu wasio na imani;
hawatashikamana nami.
4 dMoyo wa ukaidi utakuwa mbali nami;
nitajitenga na kila ubaya.

5 eKila amsingiziaye jirani yake kwa siri,
huyo nitamnyamazisha;
mwenye macho ya dharau na moyo wa kiburi
huyo sitamvumilia.

6 fMacho yangu yatawaelekea waaminifu katika nchi,
ili waweze kuishi pamoja nami;
yeye ambaye moyo wake hauna lawama
atanitumikia.

7Mdanganyifu hatakaa
nyumbani mwangu,
yeye asemaye kwa uongo
hatasimama mbele yangu.

8 gKila asubuhi nitawanyamazisha
waovu wote katika nchi;
nitamkatilia mbali kila mtenda mabaya
kutoka mji wa Bwana.
Copyright information for SwhNEN