Psalms 104:19-23


19 aMwezi hugawanya majira,
na jua hutambua wakati wake wa kutua.
20 bUnaleta giza, kunakuwa usiku,
wanyama wote wa mwituni huzurura.
21 cSimba hunguruma kwa mawindo yao,
na kutafuta chakula chao kutoka kwa Mungu.
22 dJua huchomoza, nao huondoka,
hurudi na kulala katika mapango yao.
23 eKisha mwanadamu huenda kazini mwake,
katika kazi yake mpaka jioni.
Copyright information for SwhNEN