Psalms 105:28-37

28 aAlituma giza na nchi ikajaa giza,
kwani si walikuwa wameyaasi maneno yake?
29 bAligeuza maji yao kuwa damu,
ikasababisha samaki wao kufa.
30 cNchi yao ilijaa vyura tele, ambao waliingia
hadi kwenye vyumba vya kulala vya watawala wao.
31 dAlisema, yakaja makundi ya mainzi,
na viroboto katika nchi yao yote.
32 eAlibadilisha mvua yao ikawa mvua ya mawe,
yenye umeme wa radi nchini yao yote,
33 fakaharibu mizabibu yao na miti ya tini,
na akaangamiza miti ya nchi yao.
34 gAlisema, nzige wakaja,
tunutu wasio na idadi,
35wakala kila jani katika nchi yao,
wakala mazao ya ardhi yao.
36 hKisha akawaua wazaliwa wote wa kwanza katika nchi yao,
matunda ya kwanza ya ujana wao wote.

37 iAkawatoa Israeli katika nchi
wakiwa na fedha na dhahabu nyingi,
wala hakuna hata mmoja
kutoka kabila zao aliyejikwaa.
Copyright information for SwhNEN