Psalms 106:34-39


34 aHawakuyaangamiza yale mataifa
kama Bwana alivyowaagiza,
35 bbali walijichanganya na mataifa
na wakazikubali desturi zao.
36 cWaliabudu sanamu zao,
zikawa mtego kwao.
37 dWakawatoa wana wao
na binti zao dhabihu kwa mashetani.
38 eWalimwaga damu isiyo na hatia,
damu za wana wao na binti zao,
ambao waliwatoa dhabihu kwa sanamu za Kanaani,
nayo nchi ikanajisika kwa damu zao.
39 fWakajinajisi wenyewe kwa yale waliyotenda;
kwa matendo yao wenyewe wakajifanyia ukahaba.
Copyright information for SwhNEN